𝗕𝗘𝗡𝗖𝗛𝗜𝗞𝗛𝗔 𝗔𝗡𝗔𝗛𝗜𝗧𝗔𝗝𝗜 𝗠𝗦𝗛𝗔𝗠𝗕𝗨𝗟𝗜𝗔𝗝𝗜 𝗠𝗣𝗬𝗔 𝗛𝗔𝗥𝗔𝗞𝗔
Kocha Mkuu wa Simba Abdelhak Benchikha amewataka viongozi wa Simba kuhakikisha
wanakamilisha usajili wa mshambuliaji mpya kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa
Januari 15
Baada ya kuiongoza Simba kutinga fainali ya kombe la Mapinduzi kwa ushindi wa mikwaju ya penati3-2 dhidi ya Singida FG baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1, Benchikha amesisitiza kuwa bado Simba inahitaji mshambuliaji bora zaidi ya alionao
Mmoja wa viongozi wa Simba aliyeko kwenye jopo la usajili amefichua kuwa Benchikha amekuwa mkali kupita wakati mwingine wowote
Ametaka kujua mchakato wa usajili wa mastaa wawili anaowataka haswa pale kwenye
safu ya mbele umefikia wapi huku akisisitiza mshambuliaji wa kati anatakiwa kutangulia fasta kwani waendako ni kugumu na hawawezi kutoboa kwa picha aliyoiona mpaka sasa kwenye Kombe la Mapinduzi.
Benchikha amewaambia haridhishwi na viwango vya washambuliaji wake wakiongozwa na Jean Baleke na Mosses Phiri
Baleke amefunga mabao mawili ndani ya mechi tarno alizocheza kwenye mashindano hayo huku Phiri akifunga bao moja.
"Kocha anataka matokeo mazuri zaidi anaona bado nguvu yetu kule mbele haimfurahishi tunapambana kutafuta mtu wa
maana Wa pale mbele ili hawa tulionao wawe Watu wa kuja kuongeza kitu baadaye na sio
kuwategemea kama chaguo la kwanza," alidokeza kiongozi huyo Wa Simba
Benchikha akizungumzia mechi hiyo ya jana amesema kikosi chake kimecheza mechi moja ngumu ya ndani dhidi ya timu
Bora ambayo imempa nafasi ya kujua maboresho zaidi ambapo Sasa anakwenda kutafanyia kazi.
"Hii ni mechi Moja ngumu dhidi ya timu Bora, ukipata kipimo cha namna hii kinakupa nafasi ya kujua kazi mnayofanya ina ubora
wa namna gani au wapi mnatakiwa kuongeza kitu," amesema Benchikha
"Kuna maeneo tunahitaji kuongeza nguvu au Kuna wachezaji wanatakiwa kuongeza kasi ya kutupa ambacho timu inahitaji, changamoto yetu kubwa ipo hapa tutaendelea kufanya
kazi ya kuboresha mambo ambayo tumeyabaini"

0 Comments