Ticker

6/recent/ticker-posts

RADIO ONE

SABABU 7 KWANINI HUPATI PESA MTANDAONI NA NINI UFANYE

Tuko kwenye ulimwengu ambao watu wengi tunatumia mitandao na internet. Je unaingiza pesa kupitia mitandao? Huku ni sehemu ambayo unaweza kutengeneza pesa nyingi ukiwa serious. Kwanza sasa hivi biashara zenye wateja wengi mizizi yake ni online. Wewe unafanya nini utengeneze pesa online? Kuna mtu hajawahi hata kuserch google How to make money online. Yaani ata video yangu youtube niliyoweka ya kutengeneza pesa mtandaoni haina views 2K. Anza kwa kutafuta maarifa. . Mimi sijawahi kufanya kazi ya ajira zaidi ya miezi 6 sababu online inalipa na nimeanza kutengeneza pesa mtandaoni hata kabla watu hawajaanza kunijua kwaio kuwa na jina au followers wengi si kigezo cha lazima. Unaweza pia. .. Umewahi kutengeneza pesa mtandaoni? Kivipi? .. Kuna sehemu unakwama tukusaidie? SABABU 7 Kwanini hupati pesa mtandaoni na nini ufanye 1 HUNA KITU UNACHOUZA/HUJUI KUUZA
Hupati pesa mtandaoni kwa kudownload Kama picha,ni lazima uwe na kitu unacho uza kama bidhaa,ujuzi,huduma,au kipaji na ujue namna ya kuuza 2 UOGA Kuhisi aibu kuwa watu watakuonaje ukianza kupost ,ukianza kuonyesha kipaji chako Ukianza kuonyesha ujuzi.Aisee Huku mtandaoni wanaotengeneza pesa zaidi ni walioweka uoga na aibu pembeni 3 HAKUNA TATIZO UNALOTATUA Hakuna anaye gawa pesa mtandaoni ni lazima kuwe na tatizo unalotatua ili watu watoe pesa yao.jiulize utamsaidia Nini Mtu Mtandaoni ili atoe pesa yake akupe?
4 HUJUI MITANDAO INAVYOFANYA KAZI Kama kazi yako Kupost Tu basi Sahau kuuza wala Kukuza Page Yako,jifunze Kuuza Kupitia Kuburudisha,Kuelimisha na Kutoa elimu Ili watu Watembelee Page Yako Na kuvutiwa Na Page Yako 5 HUJUI KUTUMIA TOOLS ZA MITANDAO VIZURI umewahi kutafuta Page zinazo uzwa Mfano Laptop Mtandaoni alafu Baada ya Hapo ukaanza Kuona Sponsored Ads ya Wauza laptop? Sasa Unapaswa Kujifunza namna ya kufanya watu ambao wanatafuta kitu unacho uza wakione jifunze pia kuuza kupitia Facebook sehemu Kama marketing place, group sponsored ads.nk
6 HUJUI SEHEMU SAHIHI ZA KUUZA UJUZI WAKO Mitandaoni Kuna apps Nyingi Unazoweza kufanya Kazi za Tafsiri, proofreading, Graphics,Video editing, writing.nk na ukalipwa vizuri.jifunze kutafuta Hizo apps zitakusaidia . 7 KUKOSA MUENDELEZO Kutengeneza pesa mtandaoni sio jambo la haraka kwani Unapaswa kuaminika au kujua mbinu bora za kuteka soko haraka.tatizo wengi Hutaka Akipost leo Basi Leoleo Apate Follows Wengi na Auzie wengi, Mtandaoni Kunahitaji Muda iwe Instagram.youtube, au app za freelance Ukiamua kufanya Basi fanya kwa muendelezo mpaka uone pesa 💰
Pakua app Ya MAHUMBIMEDIATZ HAPA

Post a Comment

0 Comments