
HISIA ZA KUJIONA MKOSAJI MUDA WOTE/HISIA ZA KUJIONA HAUPENDWI/HAUTAKIWI NDANI YA FAMILIA
Mwanamke au mwanaume ambaye huwa mwenye wivu wa mapenzi uliopindukia huwa anaonyesha tabia hizo kwa sababu ya hisia za kujiona hatakiwi,hapendwi,hana thamani wala umuhimu wowote kwa Mwenza wake au Watu wengine.
Hisia za kujiona hautakiw,haupendwi, hauhitajiki ndani ya familia au kwa mwenza wako zinaweza kusababisha mtu kuonyesha tabia kama vile kuomba msamaha mara kwa mara hata kama hajafanya makosa yoyote,kujali sana mahitaji ya watu wengine, kunyenyekea sana muda wote, kuogopa ugomvi au kupishana kauli na mtu yeyote,kujitoa mhanga saa 24 ili kuwafurahisha Watu wengine, kuvumilia sana vipigo, matusi, kugombezwa, kukaripiwa, kupelekeshwa, fumanizi za mara kwa mara ili kuzuia mahusiano kuvunjika.
Watu wenye hofu ya kuachwa mpweke, Watu wenye hofu ya kuumizwa hugawanyika mafungu mawili
1.Narcissist - Kundi hili linahusisha watu wenye tabia za ubabe, ukali kupitiliza, kiburi majivuno, jeuri, ujuaji, misimamo mikali sana (rigid),mtu ambaye hashauriki, haambiliki, anakuwa mjuaji sana,anakuwa mchoyo sana,anaogopa kukataliwa lakini yeye anaomba kitu chochote kwa kugombeza na kutoa vitisho,anakuwa king'ang'anizi sana wa kile ambacho anaamini,hakubali makosa wala mapungufu yake,haombi msamaha hata akifanya makosa makubwa sana anageuza kibao kwa watu wengine,akikosewa anataka kuombwa msamaha saa 24 kwa maana anataka kusujudiwa saa 24,siku zote anataka kuungwa mkono kwa kila kitu ambacho anaamini,kama ukipishana naye kauli kwa jambo lolote unageuka adui papohapo,ikiwa unamuunga mkono kila siku anataka uishi vile ambavyo yeye mwenyewe amepanga,siku zote anataka kuwa na kauli ya mwisho kwa kila kitu.
2.Borderline person: Huyu anakuwa anasifika kwa wivu wa mapenzi uliopindukia,anapiga simu mfululizo, kutuma sms mfululizo, kupiga magoti, kumbembeleza sana,anaweza kuhonga fedha nyingi sana ili kumfurahisha mwenza wake lakini anakuwa na hofu ya kuachwa mpweke,anakuwa king'ang'anizi sana,anakuwa mkali kupitiliza vilevile ndani ya muda mfupi anaanza kulia, kuomba msamaha, kutishia kujiua,anakuwa na chuki, kinyongo,wivu,anakuwa na gubu, kisirani, atasusa, atanuna, anatishia kumuacha mwenza wake mara kwa mara lakini anakuwa hana ujasiri wa kufanya hivyo.
mara kwa mara kama ni mwanaume anaweza kumpiga, kumtukana, kumkashifu, kumkaripia, kumgombeza, kumtangaza vibaya, kumlaumu, kumdhalilisha sana mwenza wake lakini anakuwa anafanya hivyo ili kuzuia mahusiano kuvunjika.
mahusiano yenye ugomvi na migogoro ya mara kwa mara huwa yenye kuwakutanisha Watu hawa wawili.
tuangalie mifano ifuatayo
1.MWANAUME (Borderline personality) & MWANAMKE (Narcissist personality)
Tuangalie hapa
mwanaume ambaye anakuwa na Borderline personality anakuwa na hisia kali sana za mapenzi kwa Mwanamke kwa maana akipenda anapenda sana kiasi kwamba hawezi kuishi bila huyo Mwanamke na vilevile ikitokea mahusiano kuvunjika anakuwa tayari kuua au kujiua ili kuepuka maumivu ya mahusiano kuvunjika.
Mwanamke (Narcissist personality) huwa wanasifika kwa uchoyo, ubinafsi,hawana huruma hata chembe,anakuwa gold digger,anakuwa yupo kimaslahi zaidi,anakuwa boss lady,anakuwa na matumizi mabovu sana ya fedha,hatosheki na mwanaume mmoja.
Tuangalie mfano hapa Mwanamke mwenye Narcissist personality anapokuwa single mother ambaye ametelekezwa na ujauzito au watoto,atakuwa na kiburi, majivuno, jeuri,, ujuaji,anakuwa na hasira kupitiliza,anakuwa na misimamo mikali sana,anakuwa hataki kuambiwa makosa yake, hataki kukosolewa, hataki kupangiwa cha kufanya sasa hapo anapokuja mwanaume ambaye ni Borderline personality inakuwa hivi.
Mwanaume anakuwa amevutiwa kimapenzi sana na Mwanamke huyo bila kujali afya ,hali ya uchumi, historia ya Mwanamke husika,hivyo mwanaume anakuwa yupo tayari kutoa fedha nyingi sana ili kumfurahisha Mwanamke (Narcissist personality).
matokeo yake mwanamke atamwambia ili uwe na mimi nataka -unijengee,unisomeshe,unitaffutie kazi,ununua nguo na simu za gharama,nataka unifungulie biashara,nataka mama na ndugu zangu uwajengee.
Kwa sababu huyu mwanaume (Borderline personality) anakuwa tayari kuvumilia kitu chochote na kufanya kitu chochote anakubali.
baada ya Mwanamke (Narcissist personality)kusimama vizuri kiuchumi,akiwa amependeza,akiwa na kazi nguzo na vilevile amejengewa, kufunguliwa biashara, kusomeshwa,watoto zake wanasomeshwa shule za gharama.
Huanza kutafuta wanaume tofauti tofauti wa kufanya nao mapenzi,hapo anaweza kukumbana na fumanizi za mara kwa mara lakini haombi msamaha wala hakubali makosa hivyo anageuza kibao kwa mwanaume (Borderline personality)
kwa muda mrefu sana anaweza kutoroka kwenda nyumbani kwao mara kwa mara,kisha anaweza kushirikiana na mama yake pamoja na ndugu zake kumgeuka mwanaume (Borderline personality) ,anaweza kurudiana na ex wake ambaye walizaa naye ,kisha anatelekeza mwanaume (Borderline personality) ambaye amejitoa mhanga kumfariji, kumlinda, kumliwaza, kumtetea kipindi alikuwa na maisha magumu sana.
kutokana na maumivu makali sana moyoni mwa mwanaume (Borderline personality) hufikia maamuzi ya kuwachuki single mother wote ,au kuamua kujiua au kumuua huyo Mwanamke (Narcissist personality) atafanya hivyo kama kisasi.
2.MWANAUME (Narcissist personality) & MWANAMKE (Borderline personality)
Tuangalie mfano mwingine hapa.
Sifa za mwanaume (Narcissist personality) ni zilezile Kiburi, majivuno, jeuri, ujuaji, misimamo mikali,anakuwa na tabia kumwambia Mwanamke (Borderline personality) kwamba "Hauna akili",, "unanuka sehemu za siri",,,,,,"mbwa",,,,,,nikikuacha hauwezi kuishi bila mimi na hauwezi kupata mwanaume wa kukuokota ",,,,,"upo na mikosi na laana"
hizi zinakuwa kauli zake za mara kwa mara.Zingatia kwamba mtu yeyote ambaye ni "Narcissist/Narcissistic personality) huwa hana huruma na furaha yake ni kuona machozi kwa mwenza wake.
Hivyo mwanaume huyu anaweza kuwa hana kazi,hana biashara,akipewa mtaji anakula, akitafutiwa kazi anatafuta kisingizio cha kuacha kazi, kutwa kucha anashinda kijiweni kupiga stori kisha akirudi nyumbani jioni anaanza kufoka, kutukana, kutoa vitisho, kuvunjavunja vitu,kumpiga sana na kumdhalilisha, kumuingilia kinguvu Mwanamke (Borderline personality) .Hii inakuwa tabia yake ya miaka yote.
Mwanamke anaweza kumfungulia biashara, kumtafutia kazi, kumnunulia zawadi za gharama,kumchukulia mkopo, kumjengea lakini kazi ya mwanaume inakuwa kubadilisha wanawake mara kwa mara,analeta wanawake kwenye kitanda ambacho analala na mwenza wake (Mwanamke mwenye Borderline personality).
kisha anaweza kubadili hati miliki ya mali zote za Mwanamke (Borderline personality) kisha anamfukuza Mwanamke wake usiku wa manane bila huruma.
lakini kwa sababu Mwanamke (Borderline personality) anakuwa na hisia kali sana za mapenzi kwa mwanaume huyu anaweza kusamehe makosa yote na kuendelea kuwa king'ang'anizi bila kujali maumivu ambayo anakuwa anapitia .
Ni vigumu sana kuwatenganisha mwanamke au mwanaume mwenye (Narcissistic personality) kwa mwanaume au mwanamke mwenye Borderline personality.
Chanzo cha tabia ya kujiona mkosaji,kujiona haupendwi, hauhitajiki ndani ya familia ni
1.Kupata baba au mama dikteta,hii inahusisha vipigo, matusi, kugombezwa, kukaripiwa, kutolewa dosari za muonekano, kunyimwa chakula, kufukuzwa nyumbani usiku wa manane mara kwa mara,kukosa wa kukusikiliza tangu utotoni, kutengwa, kubaguliwa ndani ya familia kwa muda mrefu sana huku watoto wengine wanapata upendeleo kupitiliza husababisha mmoja anakuwa Borderline personality yule ambaye amepitia manyanyaso ndani ya familia,kisha yule ambaye alipewa upendeleo kupitiliza ndani ya familia hugeuka kuwa Narcissist.
0 Comments