JIFUNZE SIRI ZA AKILI YA KITAJIRI

Masomo 20 Kutoka Kwenye Kitabu "Siri za Akili ya Milionea" (“Secrets Of the Millionaire Mind”) cha T. Harv Eker
1. Kama hufanyi vizuri kama ambavyo ungetaka kufanya, hiyo inamaanisha kuwa kuna jambo ambalo hulijui.
2. Siyo kile ambacho hatukijui kinachotuzuia kufanikiwa; ni kile tunachokijua ambacho hatujakifanyia kazi ndicho kikwazo kikubwa.
3. Kama unataka kupanda ngazi ya juu ya maisha yako, unatakiwa kuwa tayari kuacha baadhi ya namna zako za kale za kufikiri na kuishi na kuasili mpya.
4. Nina msemo: "Haitoshi kuwa sehemu sahihi kwa wakati sahihi. Unapaswa kuwa mtu sahihi, mahali sahihi kwa wakati sahihi."
5. Siri ya mafanikio ni kujitia nguvu mwenyewe; utakapofanya hivyo, watu watavutwa kwako. Na watakapokujia watoze.
6. Ulimwengu una sehemu nne ambazo ni ulimwengu unaoshikika(physical world), ulimwengu wa akili(mental world), ulimwengu wa hisia(emotional world) na ulimwengu wa kiroho(spiritual world).
7. Ukosefu wa pesa haukuwahi hata mara moja kuwa tatizo. Ukosefu wa pesa ni dalili tu za mambo yanayoendelea chini kwa chini.
8. Ramani ama mchoro wako wa kifedha unajumuisha kiasili taarifa au 'programu' ulizozipokea siku za nyuma, na kipekee zaidi ukiwa mtoto mdogo.
9. Hatua ya kwanza ya mabadiliko ni kujitambua. Huwezi kubadili jambo hadi pale utakapofahamu kuwa lipo.
10. Hatua ya pili ya mabadiliko ni ufahamu/uelewa. Kwa kutambua 'namna yako ya kufikiri' inapotokea, unaweza kutambua kuwa inatokea nje yako.
11. Hatua ya tatu ya mabadiliko ni kujitenga. Unapotambua kuwa namna hii ya kufikiri siyo yako, unaweza kujitenga nayo na kuchagua kati ya uendelee nayo ama uiache- kutokana na mtu uliyekuwa leo, na kule unakotaka kuwa kesho.
12. Kama motisha wako wa kujipatia fedha au mafanikio unatokana na asili ya "kutowezeshwa au hujuma" kama vile hofu, hasira, au kutaka kuonesha kuwa unaweza, fedha zako hazitaweza kukupa furaha.
13. Pesa haziwezi kukufanya kuwa kitu ambacho tayari umeshakuwa. Hakuna wazo linalokaa kichwani mwako bure.
14. Unatakiwa kuamini kuwa wewe ndiye unayehusika kutengeneza mafanikio yako, pia wewe ndiye unayehusika na maisha yako ya wastani, na wewe pekee ndiye unayejisababishia ugumu kwenye pesa na mafanikio.
15. Eneo unaloweka fokasi litaamua kile utakachokipata maishani.
16. Kama unataka kuwa tajiri, fokasi kwenye kutengeneza, kutunza/kuhifadhi, na kuwekeza pesa zako. Kama unataka kuwa maskini fokasi kwenye kutumia pesa zako.
17. Narudia tena, nishati husambaa: Ni aidha unaathiri watu ama unaambukiza watu.
18. Kukataa kuongezwa cheo na majukumu ni moja ya kikwazo kikubwa cha mafanikio.
19. Ukubwa wa tatizo hauwezi kuwa jambo la msingi - Jambo la msingi ni ukubwa wako!
20. Kuishi kwa minajili ya usalama zaidi ni kuishi maisha ya hofu.
0 Comments