
SABABU 6 ZENYE KUCHOCHEA UNASHINDWA KUMSAHAU MWENZA WAKO BAADA YA KUACHANA - UNASHINDWA KUMTOA KICHWANI
Mapenzi hayana bima wala hayana formula maalumu ambayo inafanya kazi kwa watu wote ulimwenguni.
Unaweza kuwa muaminifu, mwenye huruma, upendo, uvumilivu,kujali,kujitoa mhanga, kumfariji nyakati za huzuni kama vile misiba,maradhi na hali ngumu sana ya kiuchumi lakini mwisho wa siku mwenza wako akaondoka bila sababu zozote za msingi.
Kwa kuzingatia hilo leo tuangalie sababu 6 zenye kuchochea unashindwa kumsahau mwenza wako baada ya kuvunja mahusiano yenu.
Lakini kabla ya kujua sababu hizo 6 tuangalie viashiria vya mahusiano kuvunjika,kisha tuone mabadiliko ya mwili baada ya mahusiano kuvunjika na sababu hizo 6 za kushindwa kumsahau mwenza wako.
VIASHIRIA VYA MAHUSIANO KUVUNJIKA
Kabla ya mahusiano kuvunjika utaona viashiria vifuatavyo ambapo watu wengi huvipuuza.
1.MAWASILIANO KUPUNGUA
Pale ambapo mahusiano yanakaribia kuvunjika utaona mabadiliko ya mawasiliano baina yako na mwenza wako.
Atakaa kimya sana kuliko kawaida yake,simu hapokei, sms hajibu hakutafuti mpaka uanze wewe na ukikaa kimya bila mawasiliano yoyote hakutafuti.
Wengine huonyesha tabia hizi mbili
I.Mawasiliano hakuna kabisa.Labda mnakaa mikoa, wilaya,au nchi tofauti simu haipatikani, sms hajibu kwa wiki, wiki mbili, mwezi au zaidi hujui kama ni mzima au amekufa.
ii.Mawasiliano hayaeleweki.Huyu anafanya makusudi simu hapokei, sms hajibu, hakutafuti mpaka uanze wewe, ukikaa kimya tu anakaa kimya wiki, wiki mbili mpaka mwezi kisha pale ambapo moyo wako umepoteza matumaini juu yake ghafla anapiga simu mfululizo,anatuma sms mfululizo,anadai anakupenda kisha ukipata hisia kali juu yake anakata mawasiliano tena kama wiki, wiki mbili mpaka mwezi,hiyo inakuwa tabia yake ya miaka nenda rudi haonyeshi mabadiliko yoyote.
2.UNATUMIA FEDHA NYINGI SANA KULIKO UWEZO WAKO ILI KUMFURAHISHA MWENZA WAKO
Kama mwenza wako anataka muachane atakuomba fedha nyingi sana kuliko uwezo wako kwa makusudi kabisa ili ushindwe kumpatia kiasi hicho cha fedha apate sababu ya kuibua ugomvi kisha muachane.
Mwenza wako anapotaka muachane ataonekana na hasira kupita kiasi, huzuni sana, kunung'unika sana,kuibua ugomvi mara kwa mara, haonyeshi ushirikiano wowote,hashukuru kwa kitu chochote,anakosoa kila kitu ambacho unafanya au kumpa lengo uibuke ugomvi muachane.
3.KUKUMBUKA MABAYA YAKE MENGI KULIKO MAZURI YAKE
Pale ambapo mahusiano yako yanakaribia kuvunjika utakuwa na kumbukumbu mbaya zenye kuhuzunisha kuhusu mwenza wako kuliko kumbukumbu nzuri.
Unaweza kukumbuka matusi, vipigo, lawama, vitisho, tuhuma za uongo za usaliti,kuzushiwa uongo na kashfa za uongo kwa mambo haujafanya wala haujasema,
Atakugeuzia kibao kwa makosa yake na ahadi zake yeye mwenyewe.
Utakuwa na kumbukumbu za kudhalilishwa hadharani,kukunyima unyumba,au kuingilia kinguvu, kuingiliwa kinyume na maumbile, utakumbuka umewahi kujitoa mhanga kumfariji nyakati za huzuni lakini ulipokuwa na matatizo binafsi alijitenga na alikuacha mpweke.
Utakumbuka umesamehe makosa yake yenye kujirudia rudia ikiwemo fumanizi, usaliti, matumizi mabovu ya fedha,
4.KUGOMBANA MARA KWA MARA BILA SABABU ZA MSINGI
Pale ambapo mwenza wako anataka muachane atakuwa anaibua ugomvi bila sababu zozote za msingi.
Kwa mfano mnaweza kugombana kwa sababu ya kupishana kauli kuhusu chakula cha mchana au jioni,ugomvi unaweza kuibuka kwa sababu anataka password za simu yako asome sms,ugomvi unaweza kuibuka kwa sababu anadai unatoa harufu mbaya sehemu za siri,ugomvi unaweza kuibuka kwa sababu anadai hauna hadhi ya kuzungumza nae,ugomvi unaweza kuibuka kwa sababu anadai alikurupuka kukuchagua uwe mwenza wake,ugomvi unaweza kuibuka kwa sababu anawapa kipaumbele wazazi wake kuliko wewe nyakati zote ukimuhitaji,ugomvi unaweza kuibuka kwa sababu ya muda wa kurudi nyumbani,ugomvi unaweza kuibuka kwa sababu ya matumizi ya fedha,ugomvi unaweza kuibuka kwa sababu ya uvaaji,ugomvi unaweza kuibuka kwa sababu ya muonekano wa kila mmoja,ugomvi unaweza kuibuka kwa sababu ya mgawanyiko wa kazi za nyumbani,ugomvi unaweza kuibuka kwa sababu ya aina ya malezi ya
watoto,ugomvi unaweza kuibuka kwa sababu ya usafi wa mwili na mazingira ya nyumbani.
5.MAHUSIANO KUENDESHWA NA JUHUDI ZA UPANDE MMOJA
Pale ambapo mahusiano yako na mwenza wako yanakwenda kuvunjika utajikuta unajitoa mhanga kwake muda wote ili kuhakikisha mnadumu pamoja
Utapiga simu mfululizo,kutuma sms mfululizo,kuomba msamaha kwa makosa yake yeye,kukaa kimya hata pale ambapo anakufokea, kukutukana, kukudhalilisha hadharani, kukuita majina yenye udhalilishaji, kukufanya ujione mzigo, kukufanya ujione hauna akili timamu utafanya hivyo ili asiondoke.
Utajikuta unajiweka karibu na ndugu zake lakini haonyeshi ushirikiano wowote,utaingia madeni ili kumfurahisha lakini haonekani kujali chochote.
Utaongea vitu vya kuchekesha chekesha lakini haonekani kufurahia zaidi anakuwa na hasira,chuki,huzuni na kuibua ugomvi mara kwa mara.
MABADILIKO YA MWILI BAADA YA MAHUSIANO KUVUNJIKA
Pale ambapo mahusiano yanavunjika utaona mabadiliko yafuatayo mwilini mwako
I.Moyo kuuma sana, moyo kwenda mbio, miguu kuishiwa nguvu, kizunguzungu, kichefuchefu, kifua kubana sana, kupumua haraka haraka sana,hisia za kuanza kulia, kujichukia, kujikosoa, kujilaumu, kutamani kumdhuru,kumuombea mabaya
II.Kutamani kujiua,tumbo kuvurugika,mwili kufa ganzi, kupaniki, kuchanganyikiwa, hasira kupita kiasi,kubeba chuki na kinyongo moyoni muda mrefu sana,kupatwa na wivu kupita kiasi,kujiona mkosaji, kujiona kituko, kujiona laana,kuona aibu,kubanwa na choo ndogo ghafla,
III Kuanza kujitenga,kukonda sana ghafla au kunenepa sana ghafla, hedhi kuvurugika, kupoteza hamu ya kula au kula sana vyakula bila mpangilio, kukosa usingizi au kulala sana mpaka unachoka, kupoteza hamasa ya kufanya kazi,kuumwa kichwa na mgongo
ZIFUATAZO NI SABABU 6 ZENYE KUCHOCHEA UNASHINDWA KUMSAHAU MWENZA WAKO BAADA YA KUACHANA NAE
Zifuatazo ni sababu 6 zenye kuchochea unashindwa kumsahau mwenza wako baada ya kuachana nae
1.UPWEKE BAADA YA KUACHANA NAE
Mahusiano yanapovunjika huwa kuna hisia za upweke, huzuni,hasira, kujichukia, kujikosoa, kujilaumu hali hiyo inakuja automatically bila kujizuia.Husababisha unaanza kujitenga, kukonda sana ghafla au kunenepa sana mpaka unaonekana mzee kabla ya umri wako hali hiyo husababisha wivu kupita kiasi na kutamani mrudiane - Wapo huanza pombe kupindukia, kuvuta bangi, kutumia dawa za kulevya,kufanya starehe,kugombana na kila mtu kazini na nyumbani
2.UNATAKA KUMBADILISHA TABIA
Sababu nyingine ni pale ambapo unataka kumkomoa mwenzi wako kwa kumfanyia vijembe, mafumbo, kejeli kwenye mitandao.Kama unataka mwenza wako wa zamani (ex) aumie kwa sababu umeachana nae utakuwa na wakati mgumu sana kumsahau.
Yale maumivu badala apate yeye yanakuja kwako wewe mwenyewe.
Utaumia zaidi kama alikuwa ni mlevi kupindukia, muathirika wa dawa za kulevya, mhalifu,alikuwa na madeni kila kona,alikuwa hana kazi yoyote,alikuwa ametelekezwa na mtoto au ujauzito kisha ulitoa fedha nyingi sana kumfariji nyakati za huzuni lakini ghafla amekuacha na kurudiana na baba wa mtoto wake.
Maumivu makali sana moyoni yatatokana na uwekezaji mkubwa sana ambao umefanya kwake kuliko upendo ambao upo nao kwake.
Utajuta kwa sababu ya fedha, nguvu na muda ambao umejitoa mhanga kwake.
3.UMEWEKEZA FEDHA, NGUVU, MUDA MREFU SANA KWAKE
Kitu kingine chenye kusababisha unashindwa kumsahau mwenza wako baada ya kuachana ni kumbukumbu za kujitoa mhanga kwake kwa uwekezaji mkubwa sana kwa mfano alikuwa hana kazi yoyote, alikuwa ametelekezwa na mtoto au ujauzito,alikuwa hajasoma,alikuwa na madeni kila kona,alikuwa mgonjwa sana halafu juhudi kubwa sana za kuboresha maisha yake ulifanya kwa kuamini atakupenda sana kwa WEMA ambao umemfanyia
4.KUZAA WATOTO PAMOJA
Wakati mwingine ugumu wa kumsahau mwenza wako unakuja kwa sababu ya watoto ,labda watoto wamefanana nae kila kitu ukiona sura ya mtoto inakuja sura ya mwenza wako hali hiyo husababisha wivu kupita kiasi,hasira, uchungu, moyo kuuma sana kama umeachana nae kwa ugomvi mkubwa sana, fumanizi,au amekusaliti,au ameolewa au kumuoa rafiki yako wa karibu.
5.HOFU YA KUANZA UPYA BILA YEYE
Wakati mwingine ugumu wa kumsahau mwenza wako unakuja kwa sababu ulikuwa UNAMTEGEMEA kwa kila kitu hivyo baada ya kuachana unaanza upya .
Kwa mfano nyumba, usafiri, chakula na mahitaji yako yote umepata kwake na ulikuwa hauna kazi yoyote ya kuingiza fedha hivyo hofu ya kuanza sifuri mpaka ufanikiwe kurudi kwenye hali nzuri ya maisha husababisha taswira ya mwenza wako inakuja kichwani mara kwa mara.
6.KAMA BADO UNAMTEGEMEA
Ugumu wa kumsahau mwenza wako unaweza kujitokeza kwa sababu bado mwenza wako ndiyo MSAADA wako mkuu wa kuendesha maisha yako.
Kwa mfano kuna mtoto halafu mtoto amebaki kisingizio cha kupata mahitaji yako ya kila siku hali hiyo husababisha mvutano wa mara kwa mara kuhusu gharama za kumhudumia mtoto jambo ambalo husababisha unapata ugumu sana kujenga familia mpya na mtu mwengine wakati huohuo upo na ugomvi wa mara kwa mara na baba au mama wa mtoto wako.
0 Comments