YANGA ATAKWENDA ROBO FAINALI

Soka ni hesabu, na hesabu hazidanganyi.
Mara zote nafanya tathimini za namna hii na wengi wanapinga lakini mwisho wa siku mambo yanakuwa kama nilivyosema.
Hebu tufanye pamoja hizi hesabu;-
Kulingana na msimamo wa kundi ulivyo, hadi sasa Al Hilal na Alger ndio wanaopewa kipaumbele kusonga hatua ya robo.
Mechi zijazo, timu hizi mbili (Alger na Al Hilal) zinakutana Al Hilal akiwa nyumbani. Kumbuka mechi iliyopita Alger alikuwa home lakini alifungwa.
Al Hilal vs MC Alger (Mauritina)
Yanga vs TP Mazembe (Mkapa Stadium)
Al Hilal akishinda tu atakuwa na point 12 kwahiyo anaingia robo fainali, maana yake ni mechi muhimu sana kwa Al Hilal.
MC Alger akipoteza hiyo mechi, maana yake atabaki na point zake 4. Yanga akishinda dhidi ya Mazembe kwenye dimba la Mkapa, atakuwa na point 4. Msimamo utakuwa;-
1. Al Hilal (12)
2. MC Alger (4)
3. Yanga SC (4)
4. TP Mazembe (2)
Michezo itakayofuata itakuwa;-
Al Hilal vs Yanga SC
MC Alger vs TP Mazembe
Mechi ya Al Hilal vs Yanga nampa Yanga 90% za kushinda hiyo mechi kutokana na Al Hilal atakuwa ameshasonga hatua ya robo fainali, kwahiyo atakuwa hana cha kupoteza. Wakati huo MC Alger vs Mazembe, nampa 70% MC Alger kushinda hiyo mechi, kwa sababu hata kwenye mechi iliyopita, Mazembe akiwa nyumbani walitoka sare ya 0-0.
Baada ya matokeo ya mzunguko wa 5, msimamo utakuwa;-
1. Al Hilal (12)
2. MC Alger (7)
3. Yanga SC (7)
4. TP Mazembe (2)
Mechi za mwisho zitakuwa;-
Yanga SC vs MC Alger (Mkapa Stadium)
TP Mazembe vs Al Hilal (Stade TP Mazembe)
Wazee, semeni wenyewe. Yanga dhidi ya Alger kwenye dimba la Mkapa. Hii mechi ndiyo itakayoamua, ni MC Alger au ni Yanga SC nani atasonga hatua ya robo fainali.
Mechi itachezwa kwenye dimba la Mkapa, unadhani Yanga watapoteza hiyo game?! Iwe jua, iwe mvua, afe kipa, afe beki, asikuambie mtu, lazima Yanga washinde hii game. Wakati huo Mazembe dhidi ya Al Hilal mechi ambayo hatuiangalii sana, tumpe ushindi Mazembe.
Mwisho msimamo utakuwa;-
1. Al Hilal (13)
2. Yanga SC (10)
3. MC Alger (7)
4. TP Mazembe (5)
Kumbuka hizi ni hesabu tu kwenye soka, sio utabiri. Tusubiri dakika 90 za kila mchezo ndiyo zitakazoamua.
0 Comments