Ticker

6/recent/ticker-posts

RADIO ONE

KAKA MKIMBIE MWANAMKE AMBAYE AKIJIFANYIA KITU KWA GHARAMA ZAKE LAZIMA AKUDHIHAKI AU AKUKEJERI KWA NAMNA INAYOLETA FEDHEHA KWAKO

Kaka mkimbie mwanamke ambaye akijifanyia kitu kwa gharama zake lazima akudhihaki au akukejeri kwa namna inayoleta fedheha kwako Yawezekana amenunua mboga, chakula kisha akuambie unakula unajua hiyo hela imetoka wapi, amelipa bili ya maji/umeme basi lazima akuseme kama mwanaume ndiye anayetakiwa kulipia hizo bili yeye hana haki ya kufanya hivyo Mwanamke mbinafsi na mwenye kumtazama mwanaume kama mtu asiyetakiwa kutumia au kufurahia kile alichofanya mwanamke kwa ajili ya familia. Aliyechukua jukumu la usaidizi kama inavyotakiwa kuwa. Kaka ukiwa na mke ambaye akifanya kitu lazima akudhihakie au akudai umrejeshee hiyo pesa kwasababu yeye anaona si wajibu wake ni wajibu wako hamna mwanamke hapo. Ipo siku atakudhalilisha Kaka angu usipokee kitu cha mwanamke wa aina hiyo kwasababu atakufedhehesha ipo siku ukikosana naye kuwa analishawahi kufanya kile na kile kwako au kwenye mahusiano yenu Kaka hata kama una uhitaji gani muombe hata rafiki yako kuliko huyo mwanamke kwasababu atakudhalilisha ipo siku. Changamoto zako usimwambie kwasababu atakusaidia kwa majungu au hatakusaidia kabisa hata uwe na shida kubwa kiasi gani. Epuka mwanamke wa aina hii kama unahitaji kuwa mwenye AMANI

Post a Comment

0 Comments