Mbunge wa Iramba Mashariki, Francis Mtinga amesema atawasilisha hoja binafsi bungeni kuiomba serikali iweke siku maalum ya makundi ya wanachama wa mitandao ya kijamii ya WhatsApp kufanya mambo yao na shughuli za maendeleo kwa jamii.
Mtinga ametangaza mpango wake huo juzi kwa wanafunzi waliosoma Shule ya Sekondari Mwenge iliyopo Manispaa ya Singida ambao wapo katika kundi moja la whatsApp kutoka mikoa mbalimbali nchini baada ya kukutana na kufanya kazi ya kupanda miti katika shule hiyo.
Mtinga, amesema makundi hayo ya whatsApp yanawakusanya watu mbalimbali na baadhi yamekuwa na manufaa makubwa kwa jamii kutokana na kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo na kusaidiana.
"Baadhi ya wanachama wa makundi ya mitandao ya kijamii ya WhatsApp wanapokuwa wana jambo lao la kwenda kufanya nje, mfano ya kituo cha kazi inakuwa vigumu kwenda kwa bosi wake kuomba ruhusa kwasababu suala la group la whatsApp halitambuliki," amesema.
Mtinga amewaomba wabunge wenzake siku atakapowasilisha hoja bungeni aungwe mkono ili serikali ikubali kutenga siku maalum ya makundi hayo.

0 Comments