
Njia 5 Za Kuvutia Pesa Kwenye Maisha Yako 4
1
Njia 5 Za Kuvutia Pesa Kwenye Maisha Yako.
Pesa ni kitu chenye thamani kubwa kwenye maisha ya sasa.
Bila ya pesa kwa maisha ya sasa ni majanga mazito sana.
Unaweza ukakosa vitu vyote vizuri.
Hata watoto wazuri utabaki kuwaita shemeji tu.
Hotel kubwa utabaki kuziangalia kwa nje tu.
Utashindwa hata kwenda kunywa kasusi kidogo..
Pesa huwa haitafutwi bali inategwa na ndo maana kuna kitu kinaitwa "Vitega uchumi."
Unatakiwa kuwa na vitega uchumi vingi ili uweze kuwa na Uhuru wa kifedha.
Kitu cha pili kuhusu pesa ni uwezo wa ubongo kuhimili fedha.
Panua uwezo wa ubongo wako kumiliki pesa.
Kama usipopanua uwezo wako wa kuhimili pesa.
Unaweza kupata pesa nyingi na zote zikapotea.
Kwenye kutafuta pesa kuna mambo makubwa matano.
1. Kutafuta pesa.
2. Kuhifadhi pesa.
3. Kutumia pesa.
4. Kuzalisha pesa
5. Kuwekeza pesa.
Kila hatua ina mambo yake maalumu ya kufanya ili uweze kuwa bora kwenye pesa.
Leo nataka nikupe kanuni za kuweza kuvutia pesa kwenye maisha yako.
Tutatumia vitu vitano tu.
Kitu Cha Kwanza.
Mahusiano yako na pesa.
Mahusiano ni kitu muhimu sana kwenye kufanya kila kitu.
Mahusiano ni namna mtu anavyochangamana na vitu vinavyomzunguka.
Mahusiano ni tofauti na mapenzi.
Mahusiano ni namna ya kuchangamana na kitu.
Halafu mapenzi ni namna ya kukipenda kitu.
Unaweza kuhusiana na kitu bila hata ya kukipenda.
Hutakiwi kuipenda pesa unatakiwa kuwa na uhusiano mwema nayo.
Pesa unatakiwa kuheshimu na sio kuipenda.
Ukiheshimu pesa na yenyewe itakuheshimu.
Kupenda pesa ni chanzo cha mabaya yote.
Zingatia neno "Kupenda"
Timetheo 10:6 inakataza kupenda pesa.
Pesa unatakiwa uiheshimu sana.
Unaweza kuheshimu kitu bila kukipenda.
Kuheshimu maana yake ni
1. Kutafuta pesa kwa nidhamu kwa njia za heshima.
Ukiipenda pesa unaweza kufanya mambo ya hovyo sana ili mradi tu uweze kupata pesa.
Tafuta pesa kwa heshima.
2. Tumia pesa kwa heshima.
Ukipata pesa kwa heshima basi inatakiwa sana kuitumia kwa heshima.
Huwezi kutumia pesa kwenye kutweza utu wa watu.
Kuna baadhi ya watu wana matumizi ya hovyo sana kwenye pesa zao.
2. Kutunza kwa heshima.
Ukitafuta pesa kwa heshima basi utaweza kuitunza pia kwa heshima.
Itunze pesa yako kwa heshima sehemu salama.
Kuna baadhi ya jamii wanaamini pesa ina roho na huwa na kawaida ya kumuadhibu mtu anayeivunjia heshima.
Mimi ninachoamini pesa iko na energy ndani yake.
Hii energy inaweza kuwa positive au negative kulingana na wewe mwenyewe.
Lakini ukichunguza kwa karibu watu wengi walokuwa na mahusiano mabaya na fedha
Mwisho wao sio mzuri sana.
Chunguza!
Jambo la Pili.
Kanuni Ya Mvutano.
Hii kanuni ni kanuni muhimu sana kwenye maisha ya kila siku ya binadamu.
Kwa English inaitwa Law of attraction.
Hii ni kanuni ya kuvutia vitu vizuri au vibaya vije upande wako.
Kwa kuwa tunazungumzia kuvuta pesa basi hii kanuni itajikita zaidi kwenye hilo eneo.
Unaamini nini kuhusu pesa???
Je pesa kwako ni nin??
Imani yako juu ya pesa ni kitu muhimu sana.
Ukiwa na imani kwamba pesa ni kitu kibaya basi huwezi kuipata.
Ukiwa na imani pesa ni watu wa aina fulani tu.
Na ndo wenye uwezo wa kupata pesa basi huwezi kuzipata .
Unatakiwa kuamini pesa ni nzuri na ni haki yako kuipata.
Hizi imani tumetoka nazo mbali sana mpaka hapa tulipofikia.
Kutoka kwa
• Wazazi
• Jamii
• Shuleni
• Dini
• Taifa.
Je imani yako kwenye pesa ni ipi????
Je Upo na hizi imani???
1. Pesa haitoshi Duniani?
2. Huna haki ya kupata pesa???
3. Pesa ni kwa ajili ya watu fulani tu???
4. Pesa ni chanzo cha matatizo???
5. Matajiri wote ni mafisadi???
Badili kwanza imani yako juu ya pesa la sivyo pesa haziwezi kuja kwako hata siku moja.
Au zikja basi zitakutesa sana badala ya kufurahia.
Baada ya muda mfupi zinaweza kukukimbia zote.
Badili imani zako hasi kwenye pesa kwenda imani chanya.
Hiki kitu ni kigumu lakini ukijitahidi utaweza bila shida.
Hiki kitu kimekamata subconscious mind zetu.
Sisi wafanyabiashara ubongo tunaugawa sehemu kubwa mbili.
1. Conscious Mind
2. Subconscious Mind.
Imani zote kuhusu pesa ziko kwenye subconscious mind.
Jitahidi kuzifuta hizo imani na kupandikiza imani mpya kwenye ubongo wako.
Tukiachaa na hilo tuingie kwenye jambo la tatu.
Jambo la Tatu.
Power of Affirmation.
Affirmation ni maneno ya kujitamkia mema.
Kwanini huwa tunapenda mtu ajitamkie mema.
Kwa sababu maneno huumba.
Mithali 18:21 inazungumzia nguvu ya ulimi.
Chunga sana vitu unavyotamka kwa ulimi wako.
Vitu hasi vina nguvu zaidi ya vitu chanya.
Maneno ya kukatishwa tamaa ni mengi kuliko ya kutia nguvu.
Affirmation ni kujitamkia maneno mema kila siku ya maisha yako.
Maneno ya affirmation.
• Maneno yanatakiwa kuwa chanya.
Mfano mimi ni Tajiri au mimi nina pesa nyingi.
• Yatamkwe katika hali ya sasa sio ujao.
Mfano mimi Tajiri au mimi nina pesa nyingi.
• yasiwe na aina yoyote ile hasi bali yawe chanya.
Mfano mimi ni Tajiri usiseme "Nachukia umaskini"
Ubongo unafahamu vitu kwa lugha ya picha.
Muda wa affirmation.
Muda mzuri wa affirmation ni miwili kwa siku.
• Asubuhi baada ya kuamka muda huu ni mzuri sana kwa sababu ubongo unakuwa mweupe ni Rahis kupokea jambo jipya.
• Muda mfupi kabla ya kulala.
Muda huu ni mzuri sana kujisemea maneno mazuri.
Kwa sababu Ubongo hukumbuka zaidi taarifa za mwisho kabla ya kulala.
Ukifanya hivi utaanza kuona ndoto na matukio yenye kuendana na maneno yako.
Kawaida ubongo huvuta mambo yenye kutamkwa mara kwa mara.
• Ukiwa na tafakari ya kina.
Jitahidi kujisemea maneno mazuri ukiwa kwenye tafakari za kina.
Muda huu ubongo hufanya kazi ya hali ya juu sana.
• Muda wa shida na matatizo.
Muda wa shida na matatizo ni wa kuwa nao makini mno.
Huu muda pia hufanya kazi kwa kiwango kikubwa sana.
Utumie vizuri sana.
Imani Na Subra Ya Hali Ya Juu Sana.
Fahamu affirmation Sio jambo la siku moja.
Unatakiwa kurudia mara kwa mara.
Pia unaweza kutumia ubao wa matumaini.
Huu ubao mara nyingi huwekwa sehemu ambayo unaweza kuona kila siku.
Ukiwa na vitu hivi
• Maneno ya affirmation zaidi
Mfano mimi nina pesa au mimi Tajiri.
• Picha za pesa nyingi.
Unaweka picha ili ubongo wako uweze kuona picha nyingi za pesa na kutengeneza mazingira mazuria ya kuzipata.
• watu ambao unatamani kuwa kama wao.
Kwa ufupi affirmation ni kitu muhimu sana kwenye kujenga utajiri.
Point kuu.
• Maneno chanya.
• yawe katika hali ya sasa.
• utamke asubuhi au usiku.
Jambo La Nne.
Kupenda watu.
Ili uweze kupata pesa kwa hakika unatakiwa kupenda sana watu.
Pesa haziko kwa miti wala wanyama bali ziko kwa watu.
Ukiweza kuishi na watu vizuri basi utakula mema ya nchi.
Ukichukia watu huwezi kupata pesa hata siku moja.
Jitahidi sana upende watu na watu wakupende pia.
Jambo La Tano.
Kujua namna ya kutatua matatizo ya watu au malalamiko yao.
Siku zote ukiona kuna tatizo au kuna malamiko basi ujue kuna pesa hapo.
Ni jukumu lako kujua namna gani ya kutatua hayo matatizo.
Kadri utakavyotatua matatizo makubwa ndivyo utakavyopata pesa kubwa.

0 Comments