Ticker

6/recent/ticker-posts

RADIO ONE

HUJASIKIA HII! EU Yataja Nchi 7 Salama—Tanzania Yaitupwa Tangu Enzi za Magufuli!

 UMOJA WA ULAYA WATAJA NCHI 7 SALAMA, RAIA WAKE HAWASTAHILI KUOMBA UKIMBIZI



Umoja wa Ulaya (EU) umetangaza rasmi orodha ya nchi saba duniani zinazotambulika kama “nchi salama” (safe countries), ambazo raia wake hawana sababu za msingi za kuomba hifadhi ya ukimbizi ndani ya bara hilo. Hii ni kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa na taasisi husika za uhamiaji za EU, kwa kuzingatia hali ya usalama, kisiasa, kijamii na haki za binadamu katika mataifa husika.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, raia kutoka nchi hizi saba hawaruhusiwi kuwasilisha maombi ya ukimbizi ndani ya Umoja wa Ulaya, kwani mataifa yao yanachukuliwa kuwa hayana migogoro mikubwa au ukiukwaji wa haki unaoweza kuhalalisha hifadhi ya kisiasa. Nchi hizo ni:

Kosovo

Bangladesh

Colombia

Morocco

Misri

India

Tunisia

Uamuzi huu unaenda sambamba na juhudi za kudhibiti wimbi la maombi ya ukimbizi barani Ulaya, ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakitumia mwanya huo hata kama hawatoki kwenye mazingira hatarishi.

TANZANIA ILIWAI KUWA KATIKA ORODHA HIYO, LAKINI ILIONDOLEWA

Kwa upande wa Afrika, hadi mwaka 2014, baadhi ya nchi kama Senegal, Cape Verde, Benin, Ghana na Tanzania zilikuwa kwenye orodha ya nchi salama kwa mujibu wa Ofisi ya Uhamiaji ya Ufaransa (OFII). Hii ilimaanisha kuwa raia wa mataifa hayo hawakuwa na haki ya msingi ya kupewa hifadhi ya ukimbizi nchini Ufaransa.

Hata hivyo, hali ilibadilika mwaka 2015, ambapo Tanzania iliondolewa kwenye orodha hiyo muda mfupi baada ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kuingia madarakani. Sababu rasmi ya kuondolewa haikuelezwa wazi, lakini ilikuwa ni katika kipindi cha mabadiliko ya kisiasa na kiutendaji nchini humo.

Tangu wakati huo, Tanzania haijarudishwa tena kwenye orodha hiyo, licha ya kwamba hali ya utulivu na maendeleo imeendelea kuimarika kwa kiasi kikubwa katika miaka ya hivi karibuni.

Kwa maana hiyo, Tanzania kwa sasa haitambuliki kama "safe country" kwa viwango vya Umoja wa Ulaya, lakini hali halisi ya kisiasa na kijamii imeendelea kuonyesha kuwa ni nchi ya amani na utulivu.


Post a Comment

0 Comments