Kipande cha 1: Mwanzo wa Laana
Usiku wa manane kijiji cha Nyamakuta kilijikuta kimetanda na giza zito lisilo la kawaida. Upepo ulivuma kwa fujo, ukibeba harufu ya damu na moshi. Mbwa walibweka bila mpangilio, kama wanazungumza na pepo wasioonekana.
Ndani ya kibanda cha udongo, Mama Yona, mjane wa miaka 38, alitetemeka huku akimkumbatia mwanawe mdogo, Subira, aliyekuwa na homa kali. Tangu mumewe Yona afariki kwa ajali ya kutatanisha, maisha yao yaligeuka kuwa mateso ya kila siku. Kila aliyejaribu kuwasaidia alipata balaa. Watu waliamini kuna mkono wa kichawi katika familia hiyo.
Katika kijiji hicho, jina la Familia ya Yona lilikuwa mwiko kulitamka usiku. Wengine walidai familia hiyo iliingiliwa na roho za kisasi toka enzi za mababu walioua kwa tamaa ya ardhi ya ukoo.
Lakini siku hiyo, msiba mpya ulikuwa njiani.
Wakati Subira akikohoa hadi kutoa damu, mlango wa kibanda uligongwa kwa nguvu. Mama Yona alishtuka. Aliinama chini ya godoro na kuchomoa kisu alichokificha kwa miaka mitano. Akanyata hadi mlangoni...Ghafla mlango ulivunjwa kwa teke moja, na wanaume wanne waliovaa mavazi meusi, sura zimefunikwa, wakaingia kwa fujo.Mtaondoka na sisi usiku huu… au damu itamwagika!” mmoja wao aliongea kwa sauti nzito kama mtu asiye wa kawaida.
Mama Yona alijaribu kupaza sauti, lakini hakuna aliyesikia. Kijiji kilinyamazishwa kama kimelogwa.Na hivyo ndivyo safari ya mateso, damu, na laana ikaanza.
Je, nini kitatokea kwa Mama Yona na Subira? Je, hao watu weusi ni kina nani? Na kweli familia hiyo imelaaniwa?
0 Comments