Kampuni za magari za Honda na Nissan zinapanga kuungana ili kushindana vizuri dhidi ya kampuni za magari ya umeme kutoka China.
Nissan na Honda zinafanya mazungumzo ya kuungana na kuwa chini ya kampuni mama moja, ambapo makubaliano ya awali yatasainiwa hivi karibuni. Ushirikiano huu unalenga kuimarisha nafasi yao katika soko linalobadilika haraka kwa kuunganisha utaalamu wao wa kiteknolojia na rasilimali za biashara.
Japan hivi sasa imepitwa na China kwa kuuza na kutengeneza magari mengi duniani, historia ambayo zamani ilikuwa inashikiliwa na Japan. China imeitikisa Japan mpaka kampuni za Japan zimefikia hatua ya kuungana ili kukabiliana na ushindani.
Hatua hii imekuja wakati sekta ya magari duniani inabadilika kuelekea magari ya umeme. Honda na Nissan wanaamini kuwa ushirikiano huu utawasaidia kukabiliana na changamoto za kiushindani, hasa kutokana na maendeleo ya teknolojia ya umeme yanayoongozwa na Tesla na ka lolni za China.
Pia, mazungumzo yanaweza kumhusisha Mitsubishi, ambayo nayo pia imeonyesha nia ya kujiunga na kuwa kampuni tatu.

0 Comments