
KAKA UKIONA MAMBO HAYA KWA MWANAMKE WAKO MPENDE SANA
Utii wa mwanamke mara nyingi unategemea kiwango cha imani aliyoiweka kwa mwanaume wake
Mwanamke akiwa na mwanaume wanayependana sana huamini mwanaume wake humshirikisha hawezi ufanya kitu bila kumshirikisha
Kaka ukiona haya tambua unapendwa
1. Mwanamke ambaye lazima akuombe ruhusa ya mahala unapotaka kwenda na ukikataa anatii huyo anakupenda sana. Hata ukimruhusu atakuambia uwe huru kupiga simu na yeye atakuwa anawasiliana na wewe hata hamuishi naye pamoja lazima akuombe ruhusa anapotaka kwenda iwe kwenye sherehe, out nk ukisema NO imeisha hawezi kwenda na hawi na kinyongo kabisa juu kumkataza kwako
2. Mwanamke anakupendezesha yaani anakununulia nguo, vitu vya kuvaa ili upendeze. Kumbuka ana ndugu na wazazi ila hafanyi hivyo kwao anakufanyia wewe elewa anakupenda
3. Mwanamke anayekuasa kutunza akiba ya pesa zako kwa ajili ya kesho na wakati anakushauri upunguze matumizi yasiyo ya lazima analo pendo
4. Mwanamke hata ukiwa naye simu yake uko huru nayo wala haweki kindege au ikiita anaweweseka huyo ni mwanamke anayejielewa.
5. Mwanamke aliye na kipato kikubwa au hadhi kubwa ila anaiona si jambo la kujivunia au kutaka maisha ya juu akiwa kwako atakula kilichopo.
6. Mwanamke ambaye yuko tayari kuwa na IMANI moja katika ndoa (ushirika wa imani) huyo anashapevuka na anakupenda anajua misingi ya dini
7. Mwanamke utakayemkanya juu ya uvaaji wake usioupenda na akaacha bila kukuambia wewe mshamba, ninunulie nguo uzitakazo, nguo nimenunua mwenyewe nk. Akasema nitaacha kuvaa hivyo basi anakupenda
Haya ni baadhi mambo ya kujua huyo mwanamke ni tunu na dhahabu kwenye hatma ya maisha yako ya hapa duniani. Unayopaswa kuilinda na kuithamini sana usiipoteze kirahisi
0 Comments