Ticker

6/recent/ticker-posts

RADIO ONE

UNATAKA KUDHIBITI MATUMIZI YAKO? YA PESA FANYA HIVI

UNATAKA KUDHIBITI MATUMIZI YAKO? FANYA HIVI 1. Kupanga na kutumia pesa zako kwa bajeti. Hii ni njia nzuri na msingi katika kudhibiti matumizi ya fedha. Panga na usimamie bajeti yako, kuhakikisha kila pesa unayoipata inatumika kulingana na mwongozo wa bajeti yako. 2. Panga malengo ya kifedha na uishi ndani ya malengo yako. Malengo yatakuepusha kutumia pesa vibaya kwa kuwa yatakujengea mipaka na nidhamu kwenye fedha zako. 3. Epuka kununua vitu visivyo na ulazima kwako. Hapa tumia KANUNI YA SIKU 7 Kanuni hii inakutaka kabla ya kununua kitu ujipe walau siku saba (7) ili kupima uhitaji/ulazima wa hicho kitu. Ukiona kuna mambo yameshindwa kwenda kwa sababu ya kukosekana kwa hicho kitu basi ujue kina umuhimu na unaweza kukinunua. Lakini kama ukiona mambo yanakwenda bila shida yoyote basi ujue hakuna ulazima wa kununua hicho kitu hivyo unapaswa kuachana nacho. Kanuni hii ni mahsusi kwa wewe mwenye tabia ya kununua vitu bila mpangilio maalumu. Kwa kutumia kanuni hii utaokoa pesa zako nyingi ambazo huwa zinapotea kwa sababu ya kufanya matumizi holela. 4. Epuka kutembea na pesa nyingi ambazo hauna uhitaji nazo. Kamwe usiruhusu kutembea na pesa nyingi mfukoni ambazo hauna matumizi nazo kwa wakati huo. Hii itakusaidia kuepukana na vishawishi vya kutaka kununua kila kitu unachokutana nacho njiani. 5. Epuka kutunza pesa sehemu ambayo ni rahisi kwa wewe kuifikia. Mfano, kwenye simu, nyumbani n.k Pia ikiwezekana usiunganishe sehemu yako ya kutunzia pesa na mifumo rahisi ya kutolea pesa. Mfano benki na simu kupitia simu banking. Ukiweza kudhibiti matumizi yako utakuwa umeweza kupiga hatua moja mbele kuelekea kwenye mafanikio yako ya kifedha na hatimaye kufikia uhuru wa kifedha.

Post a Comment

0 Comments