Ticker

6/recent/ticker-posts

RADIO ONE

MAHUSIANO YANAKUWA IMARA PALE AMBAPO MWANAMKE ANAPOTAKA MAHUSIANO SIYO MWANAUME ANAPOTAKA MAHUSIANO

MAHUSIANO YANAKUWA IMARA PALE AMBAPO MWANAMKE ANAPOTAKA MAHUSIANO SIYO MWANAUME ANAPOTAKA MAHUSIANO Kwanini wanawake wengi huvutiwa kimapenzi na wanaume ambao hawana mpango nao wala wanaume wanakuwa hawana malengo yoyote kwa wanawake hao ? kwanini mwanaume ambaye anataka mwanamke wa kudumu naye huwa anateseka sana kwenye mahusiano? Jibu lake lipo ndani ya kitabu hiki cha JINSI YA KUPONA MAUMIVU MAKALI SANA MOYONI kisaikolojia ni kwamba mwanamke yeyote pale ambapo akiona mwanaume anaonyesha kumshobokea sana,akiona mwanaume anaomba sana namba yake,akiona mwanaume anamhitaji sana,akiona anahangaika kila kona ili ampate basi kwenye akili ya mwananmke anatafsiri kwamba huyu mwanaume hana pa kwenda , hawezi kuniacha,hawezi kuishi bila mimi. kutokana na mtazamo huo mwanamke ataanza kuonyesha dharau waziwazi,atamjibu mwanaume vibaya,atampuuza sana,atampangia sheria,atamgombeza,atamlazimisha mwanaume aishi vile mwanamke anataka . Ikitokea mwanaume amekubali kupangiwa sheria,mwanaume akiwa mpole kupitiliza,anaonyesha utii,anamnyenyekea sana,anamuomba msamaha,anambembeleza sana,mwanaume akiwa anatoa fedha nyingi sana kumjali na kumhudumia saa 24,ikitokea mwanaume anakubaliana na mawazo ya mwanamke saa 24 bila kumpinga kwa jambo lolote. Papo hapo Mwanamke anaanza kumchukia, kumdharau, kumuona tabaka la chini,kumuona mwanaume hajielewi. Haijalishi mwanaume atakuwa msomi wa kiwango cha Phd,mwanaume awe tajiri mkubwa sana,mwanaume awe na muonekano mzuri sana ilimradi mwanaume ameonyesha kujishusha sana, kumnyenyekea sana,kumuomba msamaha mara kwa mara,kukubaliana na mawazo ya mwanamke saa 24 papohapo mwanamke huyo atapoteza hisia za mapenzi kwa mwanaume huyo. kisha mwanamke huyo ataanza kuonyesha hisia za mapenzi kwa mwanaume kauzu ambaye hana mpango wa kujenga naye familia,huko mwanaamke atakubali kupigwa, kunyanyaswa, kufokewa, kutukanwa, kujibiwa vibaya, kudhalilishwa hadharani, kugombezwa, kukaripiwa, kupelekeshwa, kuingiliwa kinguvu. kwanini atakuwa mvumilivu huko na huku anakuwa mwenye dharau, majivuno, kiburi, ujuaji, misimamo mikali,anakuwa hashauriki, haambiliki, anakuwa anataka kumtawala na kumpangia sheria mwanaume mpole kupitiliza, mvumilivu, mnyenyekevu ni kwa sababu kwa asili mwanaume ni kichwa cha familia na mwanamke anakuwa chini ya mamlaka ya mwanaume tu. mwanaume akiwa mstaarabu sana anaweza kumuomba msamaha, kumbembeleza sana, kumsomesha, kumfungulia biashara, kumtafutia kazi, kumnunulia zawadi za gharama kubwa sana,kumuuguza, kuhudumia ndugu wa mwanamke,anaweza kulea watoto ambao Mwanamke ametelekezwa nao lakini kwa sababu mwanaume amempa mwanamke mamlaka ya kuwa kichwa na mwanaume amekuwa chini basi mwanamke huyo anaweza kuonyesha tabia ya kutoroka kwenda kulala na mwanaume mwengine ambaye hana mpango wa kujenga naye familia kwa sababu huku mwanaume ameonyesha tabia ya kusimama kama kichwa . Ni hulka ya kawaida kwa mwanamke kumdharau sana mwanaume ambaye anajishusha sana wake na anakuwa radhi kumnyenyekea sana mwanaume ambaye hana hisia naye wala hana mpango wa kujenga naye familia. Kwa asili mwanaume anakuwa na nguvu kwenye mahusiano pale ambapo mwanaume anakuwa hana hisia zozote kwa mwanamke. Vilevile Mwanamke anakuwa na nguvu kwenye mahusiano pale ambapo anakuwa hana hisia zozote kwa mwanaume . Mwanaume anatakiwa kuepuka kupenda ili awe na nguvu kwenye mahusiano kwa sababu mtu ambaye anapenda sana huwa anapoteza nguvu ya mamlaka kwenye mahusiano. Ukifanya uchunguzi utabaini kwamba mwanamke akishasema siwezi kumuamini kiumbe anaitwa mwanaume maishani mwangu hapo ndipo mwanamke huanza kuonyesha tabia za ubabe, ukatili, udikteta, udhalilishaji, dharau, majivuno, kiburi na jeuri akiwa na mwanaume na vilevile huo ndiyo wakati ambao mwanamke anakuwa hajali chochote kuhusu mahusiano. Ikifikia hatua ambayo mwanamke hajali kabisa kuhusu mahusiano huo ni wakati ambao Mwanamke anakuwa hatari sana anaweza kuua au kumuangamiza mwanaume muda wowote. Ukiona mwanamke hajali kabisa kuhusu mahusiano muogope.Hii ndiyo sababu mwanamke yeyote ambaye ameshajiapiza hawezi kujali mahusiano wala hawezi kukubali kuongozwa na mwanaume,wala hawezi kukubali kuwa chini ya mamlaka ya mwanaume utagundua kwamba mwanamke huyo anakuwa na uso wa hasira kupitiliza,anakuwa mbabe sana,anakuwa hashauriki, anakuwa haambiliki kwa vyovyote itakavyokuwa mwanamke akiwa na hulka hiyo huwa anaweza kuzaa kila mtoto na baba yake wala hataki kuishi na mwanaume. Kwanini mwanaume anatakiwa kuvutiwa kimapenzi na Mwanamke mpole, mwenye huruma, mwenye kujali,mwenye kunyenyekea,mwenye kujishusha ni kwa sababu Mwanamke akiwa katika hali hiyo anaweza kukubali kufuata sheria na maagizo ya mwanaume . lakini hali ya upole, huruma, kujali, kunyenyekea, kusamehe makosa, uvumilivu ikiondoka kwa mwanamke anakuwa sawasawa na mwanaume kwenye tabia jambo ambalo husababisha anakuwa tayari kuachana na mwanaume saa yoyote. Ni ukweli usiopingika kwamba katika mahusiano mtu ambaye anatakiwa kusimama na kuongoza mahusiano ni MWANAUME na Mwanamke anakuwa anatii maagizo na kuheshimu uongozi wa mwanaume. Ogopa sana Mwanamke ambaye anasema hawezi kukubali kuongozwa na mwanaume,ogopa sana Mwanamke ambaye anasema hataki kupangiwa cha kufanya kwa sababu kwa vyovyote itakavyokuwa palitokea kutoelewana katika mahusiano mnaachana muda huohuo au uishi kwa kufuata sheria zake kinyume chake mnaachana. Kosa kubwa ambalo mwanaume anaweza kufanya ni kuachia ngazi ya uongozi kwenye mahusiano hapo ndipo mahusiano yanavunjika. mwanaume unaweza kudumu na mwanamke pale ambapo mwanamke amevutiwa na wewe tu siyo pale ambapo wewe umevutiwa naye. Mwanamke anaweza kudumu na mwanaume pale ambapo yeye mwenyewe amevutiwa na mwanaume siyo pale ambapo mwanaume anaonyesha kumshobokea mwanamke. ukionyesha kumshobokea sana mwanamke lazima atakupanda kichwani,atakupangia sheria, atakulazimisha utoe fedha nyingi sana kuliko uwezo wako kisha anaweza kukuacha muda wowote wala hawezi kukumbuka wema wako kwake kwanini wanaume wastaarabu sana,wenye kunyenyekea sana mapenzi,wenye kuogopa ugomvi na migogoro,wenye kujishusha sana huumizwa kwenye mapenzi ni kwa sababu tabia hizo haziwezi kukupa nguvu ya kutoa onyo,kutoa maagizo,kukemea tabia mbaya za mwenza wako. Ukitaka mahusiano kuvunjika kama mwanaume onyesha kumshobokea sana mwenza wako, lakini kama unataka mahusiano kudumu acha mwenza wako aonyeshe kukushobokea. Akionyesha kukupenda unaweka sheria na muongozo lakini hauwezi kuweka sheria na muongozo ikiwa wewe ni mwanaume ambaye unapenda sana tena kwa hisia. Anayetakiwa kuwa na hisia kali ni mwanamke siyo mwanaume. Ikiwa umekengeuka eneo hilo basi unakwenda kulia kila siku. Mwanamke yeyote mwenye tabia ya ubabe anaijua siri hii. Mwanaume haitaji kumpenda mwanamke bali anahitaji kufanya uadilifu tu. Mwanamke hawezi kufanya uadilifu kwa sababu anaongozwa na hisia.Mtu ambaye anayeongozwa kwa hisia hawezi kumuongoza mwenzake kwenye mahusiano. Ambaye hana hisia zozote huwa mwenye nguvu kwenye mahusiano.Kama hauna hisia unaweza kumuongoza mwenza wako.Ikiwa mwanamke hana hisia zozote kwa mwanaume hugeuka dikteta kwa sababu siyo hulka ya Mwanamke kufanya uadilifu.

Post a Comment

0 Comments