Ticker

6/recent/ticker-posts

RADIO ONE

Mambo 3 ya kufanya kama mume wako ana MCHEPUKO wa kudumu na unajulikana ukweni!

Mambo 3 ya kufanya kama mume wako ana MCHEPUKO wa kudumu na unajulikana ukweni! Najua si kitu kirahisi, najua ushauri wangu ni mgumu ila una machaguo ni mawili: umuache mwanaume uondoke au ubaki naye usimfuatilie. Kama umeamua kuondoka, sikupangii ila usitishie kuondoka, yaani kama unaondoka ili uombwe msamaha inaweza kukula kwako. Lakini kama umeamua kubaki, basi ukibaki na ukafuata huu ushauri, ni miezi 3 tu wataanza kukuita mchawi kwani huyo dada atapaniki na kuchanganyikiwa. (1) Kubali kuwa huyo mwanamke ni mke mwenza, hivyo kama wana mtoto inamaanisha kabisa kuwa hata uongee nini hawataweza kuachana. Yaani kuachana kwao ni kwa wewe kuwa na amani na huyo dada kuwa na kisirani ila si kwa wewe kulalamika na kumpangia mume wako masharti. Ukikubali hivyo, inamaanisha hutajali chochote, nafsi yako itakuwa huru na hutahangaika na maisha yao. Humuambii mwanaume kuwa umekubali, bali unajiambia mwenyewe kuwa umekubali na unakaa kimya. (2) Acha kumfuatilia huyo mwanamke, acha kusikiliza umbea wowote utakaoambiwa kuhusu yeye. Maneno ya huyo dada si ya bahati mbaya; hao watu wanaojifanya kuwa ni marafiki zako, kuja kukuambia umbea wake ni wanafiki. Wengine ni watu ambao wametumwa na huyo dada au wifi zako kukutibua. Iko hivi, mwanamke wa namna hiyo alizaa na mume wako akiamini kuwa siku akimzalia mume wako atakuacha na kumuoa yeye. Baada ya kuzaa na kuona hukuachwa, akapaniki, ndiyo maana akazidisha ukaribu na mawifi, mama mkwe, kwani lengo ni kukutoa. Sasa ulipoamua kuwa na amani, akaona njia pekee ni kukufanyia vituko. Lengo ni usiwe na amani uondoke mwenyewe. Anatuma watu ili kukuambia, ana-post mitandaoni ili uone anajiweka karibu na mama mkwe, anahudhuria matukio ili uone. Lengo ni hilo tu, usiwe na amani, uiache ndoa yako kwani kwao wameshindwa kumshawishi mwanaume akuache. Mama yake amemuambia mara kibao kuwa hakutaki, mawifi washakukataa, amejilazimisha kutambulishwa ila imeshaonekana, karata pekee iliyobaki ni wewe. Sasa kama ukiendelea kuwa na kisirani mwanaume atakuacha. Narudia, ukiwa na kisirani mwanaume ataondoka, si kwa sababu anampenda huyo dada, hapana, bali kwa kuwa anachoka kujieleza kila siku kwako. Achana na simu yake, achana na kuhangaika na chochote cha huyo dada. Mwisho wa siku, utakuta dada ndiye anakua na kisirani, wanagombana, kwanini humuachi mke wako na mwanaume anamwacha huyo dada, mnakuwa na amani. Hivyo kama unataka aachwe, hupigi kelele bali unapuuza. (3) Nafikiana na mama mkwe na mawifi zako; Hao watu hawakupendi lakini hawana ujasiri wa kukuambia, wanamtumia huyo dada kuwa chombo cha kukuumiza. Sasa unachotakiwa kufanya ni kuwa mnafiki kama wao. Ukifika huko ukweni, wakikupigia simu, jifanye kama vile hujui, unayajibu salamu kama vile hujali kabisa. Hata mtu akuletee umbea, muambie hapana mimi siwezi kumuongelea mama mkwe wangu vibaya, tuachane na hayo mambo. Usijali kama wanamualika huyo mwanamke nyumbani. Hata yakitokea mambo ya nyumbani, labda msiba au sherehe na huyo dada akaja, jifanye mjinga. Yaani hata wakianzisha ushirika wewe sema tu "si mtoto wa mume wangu, hivyo hakuna shida, ni damu yao." Jifanye mjinga atachoka, yaani onyesha kuwa hata huyo dada hakuumizi, kwamba hata wakimtumia namna gani huwezi kuumizwa na mchepuko! Yaani hata akija kujisaidia huko ndani kwao, utaondoa mavi na hutalalamika. Dada, hakuna kitu kitamkimbiza huyo dada kama hicho, kwani kumbuka naye anachoka kutumika, umri unaenda, na anajiwazia kuwa yeye akizalishwa halafu kila siku hapati ahadi ya kuachwa, anaona "mhhh, nitazeekea nyumbani" ataondoka. MWISHO

Post a Comment

0 Comments