MAHUSIANO YANAKUWA IMARA PALE AMBAPO MWANAMKE NA MWANAUME WANATIMIZA WAJIBU WAO KIKAMILIFU

Mwanaume na Mwanamke siyo sawa na hawawezi kuwa sawa kwa maana kwamba 50/50 haifai na haiwezi kujenga mahusiano mazuri bali inalenga kusambaratisha familia.
WAJIBU WA MWANAUME
Mwanaume Rijali (Masculine man)anawajibika kwa mambo yafuatayo kwa mwenza wake
-Kumlisha,kumvisha, kuhakikisha Mwanamke anapata matibabu, kuhakikisha Mwanamke anapata mahitaji yake yote kwa wakati kulingana na uwezo wa mwanaume husika.(Mwanaume anatakiwa kuishi na mwanamke ambaye anaendana na kipato chake ili kuepuka migogoro ya mara kwa mara),ishi na mwanamke ambaye anaridhika na uwezo wako wa kumhudumia ili kuepuka usumbufu na ugomvi wa mara kwa mara
-Kumlinda, kumtunza,ni wajibu wa mwanaume kuhakikisha usalama wa Mwanamke upo ndani ya mamlaka yake,sio jukumu la Mwanamke kujilinda wakati mwanaume yupo, Mwanamke ni kiumbe laini,anatakiwa kulindwa kwa gharama zozote zile ili aweze kumpa mwanaume utulivu kwa ulaini wake.
Hapa inahusisha kuzuia mama mzazi na dada wa mwanaume kumshambulia, kumtukana, kumkashifu, kumkaripia, kumgombeza, kumtangaza vibaya, kumlaumu, kumdhalilisha, kumtoa dosari za muonekano,mwanaume ambaye anakaa kimya wakati ambao mama yake mzazi pamoja na dada zake wanafokea mwenza wake hafai kuendelea kuishi na Mwanamke huyo kwa sababu binti ametoka kwenye mikono ya wazazi wake kisha amekwenda kwenye mikono ya mwanaume mwengine.
Haifai kwa mama mzazi au dada wa mwanaume kumpangia binti wa watu namna ya kuishi,hafai mama na dada wa mwanaume kumtawala binti wa watu,haifai mama na dada wa mwanaume kumgombeza binti wa watu kwa sababu hana uzazi,au amezaa watoto wa kike tu,au kwa sababu ambazo wao wanaona haziwafurahishi.
-Ni wajibu wa mwanaume kumuonya mwanamke,kumpa maagizo,kumpa maelekezo.Hakuna 50/50 ndani ya familia.Mwanaume ni kichwa cha familia na Mwanamke ni msaidizi wake si vinginevyo,ikiwa Mwanamke ameanza harakati za kuleta itikadi za kimagharibi za feminist kwamba haki sawa 50/50 muondoe haraka kabla hajakuzalia mashoga na wasagaji.
Mwanaume ni kiongozi mkuu wa familia sio dikteta,haifai kwa mwanaume kumfokea, kumtukana, kumkashifu, kumkaripia, kumgombeza, kumtangaza vibaya, kumlaumu, kumdhalilisha, kumtoa dosari za muonekano mwenza wake badala yake mwanaume anatakiwa kuzungumza kwa lugha nyepesi na fasaha pale ambapo anataka kumuonya mwenza wake.Kwa mfano chumvi imezidi kwenye chakula badala ya kufoka, kutukana, kuporomosha matusi ya nguoni mwanaume anatakiwa kusema "Chumvi imezidi kwenye chakula,siku nyingine uwe makini" ,hapo mwanaume amemaliza kuongea ,hakuna kununa, kutishia muachane, kususa,kubeba chuki,kuweka kinyongo moyoni,kuanza kukumbusha makosa ya zamani hiyo haifai.
kumuongoza mwanamke ni pamoja na kuonyesha dira ya familia inakwenda wapi.
Zingatia kwamba kama wewe ni mwanaume hauwezi kujiongoza basi Mwanamke wako lazima atakuongoza.
Ikiwa hauwezi kukemea tabia mbaya za Mwanamke basi yeye ataanza kuonyesha dharau waziwazi kwa sababu atakuwa anahisi anaishi na Mwanamke mwenzake.
-Kutenda haki na uadilifu,haifai kwa mwanaume kufanya upendeleo kwa mama yake mzazi na dada zake huku anamtelekeza mwenza wake bila chakula,bila nguo ,bila fedha za matibabu,bila uangalizi wowote wakati uwezo wa mwanaume unamruhusu.
Mwanamke anatakiwa kusimamiwa na mwanaume sio kujisimamia yeye mwenyewe vile ambavyo anataka.
Hapa kuna tahadhari wapo wanaume ambao wanakuwa na chuki, kinyongo,gubu, kisirani,wivu wa mapenzi uliopindukia, anakuwa mkali kupitiliza, anakuwa mbabe sana,anakuwa mjuaji sana hizo sio sifa za mwanaume Rijali bali sifa za watoto wadogo.
Mwanaume anatakiwa kuzungumza kwa sauti nzito yenye mamlaka ndani yake Ikiwa mwanaume hawezi kumuongoza mwanamke basi atakwenda kwa bad boy na player boys ambao wataonyesha kutaka kumuongoza.
Zingatia kwamba lengo la kumuongoza mwanamke ni yeye aweze kuonyesha utii, unyenyekevu, heshima, upole, huruma, kujali na ukarimu.
Mwanamke ambaye hapati usimamizi wa mwanaume muadilifu lazima atakuwa na tabia za ubabe, ukali kupitiliza, kiburi, majivuno, jeuri na ujuaji.
Ukiona wewe ni mwanaume unataka kumbadilisha tabia mwenza wako ujue kwamba hauna sifa za mwanaume Rijali.
Ni hulka ya Mwanamke kutaka kumbadilisha tabia mwanaume ambaye hana sifa za uongozi mwanaume anakuwa mbabe,mlevi kupindukia, mcheza kamari, mhalifu, mwizi, msaliti,mgomvi mgomvi.
Mwanamke anakuwa anataka kumbadilisha tabia mwanaume aje kuwa mwanaume wa ndoto zake lakini huwa wanaambulia vipigo, matusi, kugombezwa, kukaripiwa, kufukuzwa nyumbani usiku wa manane,kupewa ujauzito na kutelekezwa.
Ukishindwa kumuongoza mwanamke utaanza kutafuta njia za kumbadilisha tabia kisha atakusumbua.
Ukiona Mwanamke hataki umuongoze achana naye kwa sababu hao huwa maalumu kwa ajili ya one night stand,kisha wanatelekezwa na ujauzito au watoto.
Epuka kuwa mwanaume mwema sana kwenye jamii bali kuwa kiongozi.
Ukiona hakuna Mwanamke yeyote ambaye anakuheshimu ni wazi kwamba hauna uwezo wa kukemea uovu kwenye jamii.
Uwezo wa mwanaume kukemea uovu na utovu wa nidhamu huwa picha ya uongozi pale ambapo anazungumza na Mwanamke.
Mwanamke akiona anajiamini sana kumzidi mwanaume huanza kuonyesha dharau,ukiona hauna uwezo wa kujiamini mbele ya Mwanamke ni wazi kwamba hauwezi kumuongoza huyu mwanamke bali huyo Mwanamke atakuwa kama mama yako mzazi kwa kukupangia sheria kila siku.
Jenga sifa za kiume ( Masculine behavior) - Hautasumbuliwa na mwanamke maisha yako yote.
Ukikosa sifa za mwanaume Rijali moja kwa moja unapoteza heshima yako mbele ya kila Mwanamke.
0 Comments