Ticker

6/recent/ticker-posts

RADIO ONE

SINGLE MOTHER

SINGLE MOTHER
Acha kuwasiliana na mzazi mwenzako wala kutamani kurudiana nae ikiwa alikataa mimba hadi mtoto baada ya kuzaliwa. Anafata nini kwako sasa ikiwa ulipamba kulea mwenyewe? mtoto amekuwa, anasoma na unaendesha maisha yako, tulia. Mpige marufuku kuja kwenu au kwako wala usiende kwake. Ni aibu kuendelea kushiriki tendo na mwanaume aliye ikana mimba ila umejifungua anakuja kujifanya kumsalimia mtoto, alikuwa wapi wakati unataabika na tumbo? Jiamin, acha kujirahisha kwa kila mwanaume kwa imani kuwa hakuna atakae kuoa na mtoto uliye nae, wewe bado ni mrembo Dada, kuzaa kumekuongea ukomavu wa akili, usijidharau kisa umezalishwa. Kaa mbali na wanaume wapita njia. Single mother epuka mazoea yanayo chochea mapenzi na waume za watu au vijana wenye uchu wa ngono wasio na mwelekeo kimaisha. Jiheshimu kuanzia uvaaji wako kauli na aina ya marafiki unao shinda nao. Ipende kazi inayo kufanya ule na kuvaa vizuri. Kuna SINGLE MOTHERS wanao jielewa na wana misimamo yao, mwanaume akimpata wa aina hii hawezi juta maana huwa mtulivu na wapo makini katika maisha. Kijana usiogope kuishi na single mother kama umemuona anakufaa. Kumbuka unapo mchukua kuishi nae huenda akabadilisha maisha yako. Single mother tulia, acha kujipendekeza kwa mzazi mwenzako ambae hana malengo nawe. Epuka kuzaa mtoto mwingine ukiwa nyumban kama bado hana nia kukuoa. Usiikate tamaa we ni mke na mama bora, subiri utapata mwanaume atae futa historia yako mbaya. Acha kujirahisha kwa waume wa watu bado unayo nafasi kupata wako. Kumbuka kuna wanawake walio zaa bila kuolewa ila wasafi wanajituza kuliko wanao jiita mabinti huku mimba kibao wametoa. Single mother endeleeni kujitunza na kujitambua, pambaneni kufa na kupona kutafuta vipato kwaajili ya maisha yenu na watoto wenu.

Post a Comment

0 Comments