
UPWEKE : FAHAMU VIASHIRIA VYA UPWEKE,VYANZO VYAKE NA MADHARA YAKE & NJIA 4 ZA UFUMBUZI
Kila mmoja huwa anajisikia upweke baadhi ya nyakati.Upweke haubagui,hauchagui unatokea kwa watu wote duniani matajiri kwa maskini,wasomi na wasiofika shule,wazee kwa vijana,waliopo kwenye mahusiano kwa ambao wapo "single" ,upweke unatokea kwa wagonjwa na wenye afya.
Utajuaje kama wewe ni mpweke ?
angalia maswali yafuatayo kujua hali yako ya upweke kisha utaangalia viashiria vya upweke
Andika NDIYO au HAPANA kulingana na hali yako
1.Sina watu wa kuzungumza nao au kufanya nao kazi pamoja?
2.Nikihitaji MSAADA huwa hakuna mtu yeyote wa kumuomba msaada?
3.Sina rafiki wa karibu?
4.Ninajiona kama nimetengwa/ nimebaguliwa?
5.Sijioni kama ni sehemu- ya jamii yangu /kikundi changu ?
6.Sina mtu yeyote wa kuongea naye ?
7.Mahusiano yangu ni ya juujuu?
8.Ninapata wakati mgumu sana kupata marafiki?
9.Sipewi mualiko popote ?
10.Ninajisikia upweke muda wote ?
VIASHIRIA VYA UPWEKE
a.Huzuni,kukosa furaha,kutamani kulia au kutokwa machozi,kujiona hauna thamani, kujichukia, kujilaumu,kuanza kuwalaumu Watu wengine
b.Kujiona tabaka la chini,kujiona laana,kujiona mkosaji,kujiona kituko,kujiona kitu cha aibu,,kujiona mzigo,kubeba chuki, kinyongo na wivu uliopitiliza,kutamani kujiua au kumdhuru mtu mwingine,hisia za kisasi.
c.Kukosa nguvu ya kufanya kazi,kulala sana mpaka unachoka,au ,kukosa usingizi,moyo kwenda mbio, kizunguzungu, kichefuchefu,hasira kupitiliza,kuumwa kichwa na mgongo,
d.kuanza kujitenga na familia pamoja na marafiki,kukonda sana au kunenepa sana, kuonekana mzee sana kabla ya umri, kupoteza hisia za mapenzi.
VYANZO VYA UPWEKE KUPITILIZA
Upweke kupitiliza unaweza kusababishwa na vyanzo vifuatavyo
a.MIGOGORO YA KIMAPENZI/MIGOGORO YA KIFAMILIA
-Ugomvi wa wazazi wenye kujirudia rudia,wazazi kuachana ghafla,wazazi kupeana talaka, wazazi kupeana kashfa na tuhuma za usaliti na ushirikina,
-kushuhudia mzazi anapigwa, kudhalilishwa hadharani, kugombezwa, kukaripiwa, kutolewa dosari za muonekano, kufukuzwa nyumbani usiku wa manane
-kumfumania mwenza wako, usaliti, kutishiana kuachana, kutukanana, kudharauliana, kushutumiana, kugombana mara kwa mara,kunyimwa unyumba kwa muda mrefu sana,au kuingiliwa kinguvu
-kugundua watoto ulidhani ni damu yako sio wa kwako.
-mwenza wako kuiba mali zako kisha akatokomea kusikojulikana,
-kugundua mwenza wako amejenga na kufungua biashara kwa siri lakini wewe huwa unamshirikisha kwenye kila jambo lako.
-mwenza wako kukuambukiza ugonjwa usiokuwa na tiba kama ukimwi kisha akatokomea kusikojulikana
-Mwenza wako kukuacha ghafla baada ya kwenda masomoni au kurudi nyumbani kwao kusalimia.
b.KUTENGANA NA WAPENDWA WAKO
upweke kupitiliza unaweza kusababishwa na kifo cha ghafla cha mpendwa wako kama vile mzazi,mwenza,mtoto,rafiki wa karibu n.k
c.KUPITIA HALI NGUMU SANA KIUCHUMI
Upweke kupitiliza unaweza kusababishwa na kupitia kipindi kigumu sana kifedha kwa sababu zifuatazo
-kukosa ajira ,kukosa kazi ya uhakika kwa muda mrefu sana huku Watu umesoma nao wakiwa na kazi na biashara nzuri na wengine wamezaa na kujenga
-kuibiwa, kufukuzwa kazi, kufilisiwa na benki,kutapeliwa, kuvamiwa na majambazi, kunyang'anywa mali,
-majanga ya asili/moto kuteketeza mali zako zote ghafla
d.MAGONJWA /MATATIZO YA KIAFYA
Upweke kupitiliza unaweza kusababishwa na kuugua kwa muda mrefu sana bila kupata nafuu,kuwa na ulemavu wa kudumu,kupata ajali yenye kusababisha ulemavu wa kudumu, kusumbuliwa na ugonjwa usiokuwa na tiba kama ukimwi kunaweza kusababisha hisia za upweke kupitiliza.
Vilevile kujichukia kwa muonekano kunaweza kusababisha hisia za upweke,pamoja na kuwa na dosari ya muonekano ambayo inakufanya ujione tofauti na Watu wengine kwenye mikusanyiko
e.MALEZI YA UTOTONI & KUMBUKUMBU MBAYA ZENYE KUHUZUNISHA
Upweke kupitiliza unaweza kusababishwa na kukua tangu utotoni bila kumuona mama au baba mzazi,kukataliwa na baba au mama mzazi, kutekelezwa na baba au mama, kudhulumiwa mali za urithi, kubaguliwa,kutengwa,kuona ndugu zako wanapewa upendeleo kutokaa kwa wazazi wako.
matukio mengine ni kama vile kupigwa, kufokewa, kutukanwa, kujibiwa vibaya, kudhalilishwa hadharani, kufanywa kichekesho,kunyimwa chakula,kulazwa chooni, kufungwa kamba kwa muda mrefu huku ndugu zako wanapendwa sana na kupewa upendeleo kutoka kwa wazazi wako.
MADHARA YA UPWEKE KUPITILIZA
Upweke kupitiliza unaweza kusababisha
-kifo cha ghafla,kujiua au kumdhuru mtu mwingine,kufanya uhalifu
-ulevi uliopindukia, uvutaji bangi, matumizi ya dawa za kulevya,kutumia fedha nyingi sana ghafla,kushiriki mapenzi na mtu yeyote ili kuondoa upweke , kubadilisha wanawake au wanaume mara kwa mara
-kugomea kazi, kuharibu haribu kazi na mali kwa makusudi ili kukomoa
-Kulala sana, kujitenga.
NJIA ZA KUKABILIANA NA UPWEKE
kutoka ndani ya kitabu cha JINSI YA KUPONA MAUMIVU MAKALI SANA MOYONI
1.PATA UTULIVU WA AKILI
Kuna njia kama kuvuta pumzi kwa nguvu kisha unaacha pumzi taratibu taratibu (deep breath exercises),kupiga miayo (yawning) -maelezo ya ziara soma kitabu cha JINSI YA KUPONA MAUMIVU MAKALI SANA MOYONI
2.TAFUTA MTU WA KUZUNGUMZA NAYE
Kuongea husaidia kuondoa sumu ,(Venting) kuongea na mtu ambaye anaweza kusikiliza bila kukukosoa, kukulaumu,kukutuhumu, kukudhalilisha - katika jamii Watu wengi hawana mawazo wala ushauri wenye kusaidia wengi ukieleza tatizo lako unageuka mada ya kujadiliwa nyuma ya mgongo kisha unachekwa kwa taarifa zako kujulikana.Chagua mtu kwa umakini
3.ANDIKA HISIA ZAKO KWENYE KARATASI
Wapo ambao upweke wao umewasaidia kuandika nyimbo tofauti tofauti,wengine mashairi n.k kila mtu na njia yake ya kueleza maumivu yake kwenye karatasi
4.TUMIA UPWEKE WAKO KAMA HAMASA
Achilia matukio yaliyopitwa na wakati, mabadiliko lazima yajitoleze iwe kwa kutaka au bila kutaka mabadiliko hayo.
"Epuka kushindana na mazingira yako kwa kupinga mabadiliko badala yake ruhusu maisha yake kama yalivyopangwa siyo vile ambavyo wewe umepanga.
ondoa hofu kuhusu namna ambavyo maisha yamekuwa juu chini (upside down).Kwani umejuaje kama aina ya maisha ambayo ulikuwa umezoea kuishi ndiyo bora kuliko maisha yanayokuja siku za baadaye?" Shamz Tabrizi
Unajifunza kutetea haki zako pale ambapo umedhulumiwa
unajifunza kujitegemea kiuchumi pale ambapo hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kukusaidia hata senti tano
unajifunza kutunza siri zako pale ambapo umesalitiwa
unajifunza kusimama kwa miguu yako baada ya Watu uliowategemea kukutelekeza ukiwa na matatizo makubwa sana
unajifunza kujali muda wako pale ambapo Watu wengine wanakutumia kwa maslahi binafsi
unajifunza kujipenda pale ambapo Watu wanakuchukia
0 Comments