Ticker

6/recent/ticker-posts

RADIO ONE

UTUNZAJI WA PESA KATIKA MAENEO MBALIMBALI

UTUNZAJI WA PESA KATIKA MAENEO MBALIMBALI Kadri mtu anavyokua kiuchumi (tajiri) ndivyo anavyoongeza idadi ya watu wanaomfuatilia na kutaka kumjua kiundani ikiwepo serikali, mashirika ya siri, idara nyeti, kampuni washindani, vikundi maalum vyenye nia mbalimbali na watu wa karibu wanaomzunguka. Kufuatiliwa huku huwa hakuhusiani na vile mtu alivyo ila huwa kunalenga kukipata kile ambacho kinamfanya mtu kuwa vile alivyo yaani pesa hata kama sababu itaanzia kwake ama iwe kesi, maradhi, kifo au kuhusishwa na hujuma fulani nk. Kutunza pesa kwenye maeneo mbalimbali ni desturi ya matajiri wengi ambayo huwa inafanywa kwa siri ili kuepuka mambo yafuatayo;- i. Pesa kutaifishwa ii. Kuchunguzwa/kufuatiliwa kimyakimya iii. Kuepusha kuingiliwa/kudukuliwa iv. Kuepusha kupoteza pesa nyingi pindi yakitokea machafuko v. Kuvamiwa au kukamatwa Utunzaji wa pesa katika maeneo mbalimbali ya kawaida na ya siri umegawanyika katika namna kuu mbili ambazo ni;- 1. NJIA ZA KIBENKI Katika kutumia njia za kibenki baadhi ya matajiri huwa wanatunza pesa kwa kuzingatia mambo yafuatayo;- i. Wanatunza pesa katika akaunti mbalimbali ili kuepusha akaunti moja kuonekana ina pesa nyingi zaidi. ii. Wanatunza pesa kwenye akaunti ya aina zaidi ya moja iii. Wanatunza pesa kwenye akaunti zenye majina ya watu ambao sio watu wao wa karibu au watu wanaofanania majina bila kujali uchukuaji wa alama za vidole na namba za siri. iv.Wanatunza pesa katika benki za kitaifa na kimataifa. Njia za kibenki sio njia zinazoaminika na za uhakika sana ila wengi huwa wanalazimika kuzitumia kwa sababu za kibiashara, malipo, ukuaji wa teknolojia na matakwa/taratibu ya serikali. 2. NJIA ZA SIRI Nje ya njia za kibenki matajiri wengi wana maeneo maalum ya ama kufungia ama kuzika pesa zao ama ardhini, kwenye maandaki au kwenye mashimo. Njia za siri ndiyo njia ambazo zimekuwa zikionekana kuwa salama na za uhakika kwa sababu hazihusishi watu wengi wala mamlaka kujua pesa/mali za thamani za mtu zilipo. Inasisitizwa kujua mapema au kuanza mapema kutunza pesa katika maeneo mbalimbali ya kawaida na ya siri kwa sababu ulimwengu wa pesa na utajiri ni ulimwengu wa vita na kuwindana kila uchwao haijalishi mtu anaingiza pesa kwa kufanya kitu haramu au kwa kufanya kitu halali.

Post a Comment

0 Comments